RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

LHRC, WADAU WA MITANDAO WAJADILI KUKUZA UTAWALA BORA

Mmoja wa wa wadau wa mitandao ya kijamii akizungumza kuhusu mitandao ya kijamii inavyoweza kukuza utawala bora.

Baadhi ya watoa mada wa mdahalo walivyoonekana meza kuu.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo, Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga (katikati) na Mwanasheria wa LHRC, William Kahale wakiwa katika mdahalo huo.

Washiriki wa mdahalo huo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.


Wakati wadau mbalimbali na wanatetezi wa haki za binadamu wakiwa wanazilalamikia kanuni mpya za maudhui mitandaoni ambazo zimetolewa hivi karibuni, bado wapo wadau wanaosema si kanuni zote zenye matatizo kwani kuna kanuni zingine ambazo zinalinda maadili na utu.

Vipengele hivyo vinahusu kulinda haki za mtoto, kuzuia matusi mtandaoni na hata kupunguza picha zisizofaa.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali wakati wakichangia mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) uliokuwa na lengo la kujadili mchango wa mitandao ya kijamii katika kukuza utawala bora

Comments