RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

08.04.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA MAOMBI YA KUKOMESHA NJAA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

"
Baadhi ya watu waliokoka katika ibada ya KUKOMESHA NJAA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 8.04.2018. Tunamshukuru sana Mungu kwa kuwaokoa watoto wake waliokuwa wakiteseka na nguvu za giza na wengine wakihangaika na magonjwa.

Mch. Francis Machichi na Mch. Maunumbu waliongoza sala ya toba, na kuwaombea watu wote waliokoka siku hiyo. Baada ya maombezi walibatizwa kwa maji mengi na siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kuanza masomo ya kukulia waokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.

Wewe ambaye hujaokoka BWANA anakuita siku ya leo ili umpokee kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako. Ndugu yangu muda ni sasa wa kumrudia MUngu wako. Kuna kipindi kitafika utatamani kuokoka lakini utashindwa, utatamani kuomba lakini utashindwa, utatamani Neno la Mungu lakini hutalipata, utatamani kuonana na watumishi wa Mungu lakini hutawapata. Muda ni sasa na sio kesho.

Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi jadi saa 8 mchana. 

Kanisa limekuandalia usafi wa bure wa kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.

 Mch. Manumbu







MCH. PRISCA CHARLES












Mch. Maina kutoka Kenya














Comments