RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

01.04.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOWAPAKA MAFUTA YALIOOMBEWA WAUMINI SIKU YA JUMAPILI YA PASAKA


Tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya katika ibada ya Jumapili ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni 'B" siku ya tarehe 01.04.2018. Katika ibada hii ya Pasaka Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwapaka mafuta yaliyoombewa kwa waumini wote wa kanisa hilo pamoja na watu wote walioshiriki ibada hiyo Takatifu akishirikiana na wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni "B.

Baada ya kumaliza kupaka mafuta baadhi ya watu walioshiriki ibada hiyo waligawiwa mafuta na kwenda nayo majumbani mwao kwaajili ya kuwapaka na wengine.

Tunapenda kukukaribishha katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana, kwahiyo wahi mapema ili upokee muujiza wako kutoka kwa BWANA. Watumishi wa Mungu wamejiandaa kukuhudumia kiroho. Unaombwa kuja na mwenzako katika ibada Jumapili hii ili naye aweze kujifunza Neno la Mungu, kuombewa na kutamkiwa baraka za Mungu kwaajili ya maisha yake na yako.

Mungu anweza kubadilisha historia ya maisha yako kwa wakati anaoujua yeye. Yawezekana Jumapili ikawa ndio siku yako ya kupokea kile ulichoomba kwa muda mrefu. Chukua hatua za kufika hemani mwa BWANA Mlima wa Moto Mikocheni "B". Nitatamani kukuona nyumbani mwa BWANA Jumapili hii. Mungu akubariki sana..


Naibu waziri wa Kilimo Mhe. Mary Mwanjelwa akipakwa mafuta na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


























































































































Comments