RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE | MAOMBI KWA WATU WENYE UHITAJI WA KODI YA NYUMBA NA ADA YA SHULE

BWANA APEWE SIFA..
Nataka nikutie Moyo wewe unayepitia changamoto ya kodi ya nyumba na ada ya shule. Umehangaika kila mahali kutafuta kodi ya nyumba na ada ya shule bila mafanikio. Kila mtu ukimuendea anakuahidi lakini hatimizi ahadi yake.

Siku ya leo Mungu atakufanyia wepesi wa kuipata hiyo kodi ya nyumba na ada ya shule, wewe amini tu. Piga magoti mlilie Mungu wa mbinguni naye atajibu kwa kishindo mpaka maadui zako washangae
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Yawezekana kuna watu wamefunga milango yako ya mafanikio ya kupata kodi ya nyumba au ada ya shule ili uabishwe na ufedheheshwe, nakusihi Jumapili hii kimbilia Mlima wa Moto Mikocheni "B" nikuombee, na Mungu ninayemuamini na aliniwezesha atafanya njia pasipo na njia.

-------------------------------------------
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" -DSM
Ibada zetu za Jumapili zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa zitaanza saa 9 alahamisi hadi saa 1 usiku.

Comments