RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.03.2018: WAHUBIRI WA KIMATAIFA KUTOKA KENYA NA BRAZIL WALIPATA KIBALI CHA KUHUBIRI KATIKA KANISA LA MLIIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

TAFAKARI:
// MITAHLI 24:5. Mtu mwenye HEKIMA ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza UWEZO; Maana mashauri huja wokovu.//

Ukitaka uongezeke KIUWEZO tamani sana kuwa karibu na watu wenye MAARIFA, watakufundisha mengi na yatakusaidia katika maisha yako. Muombe Mungu sana akukutanishe na watu wenye MAARIFA katika huduma yako, kazi yako, biashara yako, katika masomo yako n.k. ili UWEO wa maarifa UONGEZEKE. 

Unapoona unakosea jambo tamani kuomba sana USHAURI kwa watu sahihi na wenye MAARIFA watakusaidia kukupa njia bora ya mafanikio. Unapopata maarifa una uwezo wa kufanya vitu vyako kwa UMAKINI na kuchambua baya na zuri. Unapopokea USHAURI mzuri kwa watu sahihi utakuletea msimamo mzuri hata katika imani yako na wokovu wako kwasababu utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua mema na mabaya ili kufanikisha malengo yako.

Na kama unahitaji kuwa na NGUVU katika kila jambo, tamani sana kuwa na HEKIMA kwasababu mtu mwenye hekima ana nguvu. Kila jambo unalotaka kulitoa katika kinywa chako litafakari kwanza na kujua mazuri yake na mabaya yake baada ya kulitamka kwa watu. Muombe sana Mungu akupe Roho Mtakatifu wa kukuongoza katika MAAMUZI yako.

Siku ya Jumapili 11.03.2018 katika ibada ya KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tulitembelewa na wageni kutoka Kenya na Brazil. Kupitia wao tulipata maarifa ambayo yalituongezea UWEZO wa kutafakari kazi za Mungu na tulipokea HEKIMA inayotupa NGUVU katika kumtumikia Mungu. Kupitia mahubiri yao tuliona uwepo wa Mungu na pia tulipokea USHAURI kutoka kwao ambao unatusaidia kudumisha wokovu wetu na kusonga mbele katika kazi ya BWANA. maneno yao ya HEKIMA yametupa NGUVU ya kumtumikia Mungu na kupigana na huyoi mwovu shetani.

Sasa, wewe uliyekosa kufika kanisani na wewe uliyefika ibadani, tunakualika tena katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini Dar es Salaam. Siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ibada inaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku, usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini Dar es Salaam.































Comments