RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.02.2018: AMOSI AKIIMBA KATIKA IBADA YA BIG SUNDAY TO REMEMBER 2018

//ZABURI 138:1 -2. "Nitakushuru kwa moyo wangu wote, mbele ya miungu nitakuimbia zaburi. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako kwaajili ya fadhili zako na uaminifu wako kwa maana umeikuza ahadi yako kuliko jina lako lote."//

Hivi ndivyo mtumishi wa Mungu Amosi ambaye Mungu amempa karama ya uimbaji na ni mtalamu wa mambo ya muziki hasa upande wa sauti (Sound Engineer). Siku ya Jumapili 11.02.2018 katika ibada ya BIG SUNDAY TO REMEMBER iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kupata nafasi ya kumuimbia MUngu na kumshukuru kwa matendo makuu anayofanya katika maisha ya watu.. Nyimbo yake iligusa mioyo ya watu kutokana na ujumbe wake. 

Ibada hii ilikuwa ni ibada maalum kwaajili ya makasi yote ya Mlima wa Moto Tanzania ambayo yalikusanyika na kusali pamoja katika Makao Makuu ya kanisa hili yalioyopo Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam. Ibada hii huchukua masaa 12 na zaidi na siku ya Jumapili ilianza saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Ni ibada ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka.

Sasa nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. kanisa limekuandalia usafir wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa. karibuni wote.







Comments