RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: ROSEMARY MGETHA NA NDUGU ZAKE WAMSHUKURU MUNGU KWA KILICHOTOKEA KATIKA FAMILIA YAO

Katika maisha hakuna neno zuri kama kusema., "ASANTE". Ni neno dogo sana lakini lililobeba maana kubwa sana kwa yule aneayeambiwa "ASANTE" Hataka kama unapitia magumu ya aina gani wewe mshukuru Mungu na useme "ASANTE" kwa yote unayopitia. Hata kama uko katika maisha mazuri na ya starehe ya namna gani, endelea kusema " ASANTE MUNGU" kwa kuniweza. Katika mapito unayopitia usishau kumshukuru Mungu kwa kumaanisha. Mungu ndiye anayejua njia zako na hatma ya maisha yako. Mungu ndiye anayejua shida zako na jinsi ya kukupitisha katika shida zako hizo.

Hivi ndivyo Mch. Rosemary Mgetha na wanandugu walivyomshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea katika familia yao. Shukurani hizi zilitolewa siku ya Jumapili 14.01.2018 katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Walimshukuru Mungu kwa kile kilichotokea katika familia yao, na pia walimshukuru Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa upendo wake juu ya familia hiyo na jinsi alivyojitoa kushirikiana nao. Waliwashukuru wazee wa kanisa na vijana kwa kujitoa kwao kuhakikisha kili jambo linaenda sawa. Pia walimshukuru sana Mch. Noah Lukumay kwa jinsi alivyohusika katika maombi na kufundisha NENO la Mungu, na kusababisha watu waliohudhuria eneo hilo kutajabishwa na kuguswa na ujumbe wa Mch, Noah Lukumay.

Yawezekana unapitia mateso fulani au yawezekana umebarikiwa sana na unahitaji mkono wa Mungu uwe juu yako katika baraka zako au magumu unayopitia. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu anampngo na wewe katika mafanikio yako au magumu unayopitia.

















 








Comments