RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: MHE. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AFANYA MAOMBI KATIKA IBADA YA KUSHIKWA MKONO NA MUNGU

Hivi ndivyo maombi mbalimbali yalivyofanyika katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU siku ya Jumapili 14.01.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji waliweza kuwaombea waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" pamoja na wageni waliofika kuabudu siku hiyo. katika kipindi cha maombezi watu waliguswa na nguvu za Mungu na baadhi yao walianza kutokwa na majini na mapepo huku yakipiga kelele kwasababu yalikuwa yananunguzwa na moto utokao mbinguni.


Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii, watumishi wa Mungu walikuombea hapo ulipo na kukutamikia baraka. Tunatambua wengine walishindwa kufika kanisani kutokana na magonjwa, kazi, safari, kuuguza na mambo mengine kama hayo. Kwa kutambua hilo kanisa liliweza kuwaombea na kuwatamkia baraka. Lakini kuna wengine hawakuweza kufika kanisani kutokana na kufungwa na nguvu za shetani, hawakuona umuhimu wa kuja kanisani kwasababu nguvu za giza zilikuwa zikiwasumbua na kuwasukuma wasitamani kufika kanisani. Kwa kutambua hilo kama kanisa lilikuombea ili ufunguliwe na uweze kufika kanisani kwaajili ya maisha yako ya baadae huko mbinguni.

Sasa, tunakuomba wewe ambaye huna sababu yoyote ya kutofika kanisani, unaombwa sana kufika kanisani kwaajili ya kumtukuza Mungu wako aliyekuumba ili abadilishe maisha yako.

Yawezekana unajiona una kila kitu, na huoni faida ya kuja kanisani, nataka nikuambie ndugu yangu ya kuwa ipo siku utabanwa na utatamani kufika kanisani lakini utashindwa, utatamani kuombewa lakini utakosa wa kukuombea, utatamani maombi na hutayapata, utatamani kuona na watumishi wa Mungu lakini hutawapata, utatamani kuwahonga pesa watu wakusaidie lakini fedha zako hazitatatua shida yako, utatamani ukutane na nguvu za Mungu lakini itashindikana, mali zako na fedha zako hazitakusaidia.

Amua sasa kumtumikia Mungu ili kujiwekea hazina yako ya baadae huko mbinguni na pale utakapobanwa ukiwa duniani. Anza kuishi maisha ya maombi, mshirikishe Mungu kila hatua unayopitia katika maisha yako. Muweke Mungu wa kwanza kwa kila jambo. Shiriki ibada kila kuitwapo leo, uwe mtu wa toba, mtu wa kusoma Neno la Mungu na kulifanyia kazi, saidia wenye uhitaji, onyesha upendo kwa kila mtu bila ya kuangalia kipato chake. tamani maisha yako yawe mfano mzuri kwa majirani zako na ndugu zako. Achana maisha ya kutegemea waganga, wanandamu au kitu chochote mbali na Mungu. Kumbuka hapa duniani tupo kwa kitambo tu, ipo siku tutakufa. 

Nikukaribishe katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi sa 8 mchana na siku za katikati ya wiki ibada itaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.








 Mch. Noah Lukumay







 Mch. Francis Machichi (kulia) na Mzee wa kanisa Mzee Malya

Comments