RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: MCH. PRISCA ASABABISHA WATU KUGUSWA NA NGUVU ZA MUNGU ALIVYOIMBA NYIMBO ZA KUABUDU

Katika waimbaji wanaoimba na walioishi katika maisha ya wokovu tangia udogo, hutamuacha kumtaja Mch. Prisca Charles ambaye amelelewa Kiroho na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tangia akiwa mdogo sana mpaka sasa. Siku ya Jumapili 14.01.2018 katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kugusa mioyo ya watu na kuimarisha IMANI za watu kupitia uimbaji wake akishirikiana na Praise & Worship Team. hakika alishusha uwepo wa Mungu na watu waliguswa na nguvu za Mungu na wengine kusababisha kutokwa na machozi. Mch. Prisca Charles amefanyika baraka kwa kanisa kutokana na uimbaji wake na amegusa maisha ya watu kupitia huduma yake ya uimbaji.  Na hii yote ni kutokana na malezi bora ya Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kanisa zima la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wengi sana wanaopitia mikono ya mtumishiwa Mungu Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wamefanyika baraka kwa watu wengine na wamesababisha watu wengi sana kuokoka.

Waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walionekana kubarikiwa sana na "Praise & Worship Team" ikiongozwa na Mch. Prisca Charles kwa uimbaji. Tunatambua ya kuwa Mungu wetu ni Mungu wa sifa, kwahiyo siku hiyo alionekana akishughulika na kila mtu aliyefika katika ibada hiyo kupitia ibada hii ya kusifu na kuabudu.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii kwako wewe ambaye ulikosa ibada hii na wewe ambaye uliweza kushiriki ibada hii ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU. Jumapili hii ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana
Mch. Prisca Charles





























Comments