RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: KANISA LAMSAIDIA MZEE AMBAYE AMENYANG'ANYWA NYUMBA PAMOJA NA MKE WAKE.

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU iliyoongozwa na Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ambayo ilifanyika siku ya Jumapili 14.01.2018 lliweza kumsaidia mzee ambaye amenyang'anywa nyumba pamoja na mke wake na hivi sasa hana sehemu ya kuishi. Waumini baada ya kusikia habari hizi kutoka madhabahuni waliweza kumiminika madhabahuni kumtolea chochote walichokuwanacho na wengine wakitoa machozi huruma.

(Kujua zaidi tunakuandalia video ambayo utaona katika link tutakayotoa hapa.)

Watu kama hawa wapo wengi sana mitaani mwetu na wanahitaji msaada kutoka kwako. Na wengine ni nguvu tu za giza zinazosababisha haya yote kutokea. Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kibali walichopata kutoka kwa Mungu lipo kuwasaidia watu kama hawa kiroho ili wafunguliwe na waweze kupata haki zao. Wewe ambaye unapitia changamoto kama hii tunakualiaka katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B", ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanaisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. kama wewe huna hiyo changamoto basi mlete ndugu yako au jamaa yako anayesumbuliwa na Yesu atarudisha haki yake.













Comments