RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: JOSEPH KUTOKA EFATHA TEMEKE NA MARIA KUTOKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAMSHUKURU KWA KUFANIKISHA HARUSI YAO


Joseph kutoka kanisa la Efatha Temeke na Maria kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walimshukuru Mungu kwa kufanikisha harusi yao. Joseph akiongea katika madabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", alisema, anamshangaa sana Mungu kwani alikotoka ni mbali (Temeke) na akaweza kumpata mke katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wilaya ya Kinondoni, hakika huu ni ushuhuda kwake. Alimshukuru sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kumlea Kiroho mke wake na aliweza kumtania kwa kusema, "Anampenda Bishop kwasababu wanatoka mkoa mmoja wa Morogoro". Alimshukuru sana Bishop kwa kumpa mke ambaye ni mtumishi wa Mungu.

Joseph hakuishia hapo aliwashukuru wachungaji kwa upendo wao kwa kipindi chote cha maandalizi ya harusi yao mpaka walipoweza kufunga ndoa halali. Alisema katika maombi yake hataweza kuwasahau kwa wema waliomtendea pamoja na mke wake Maria.. Aliwashukuru sana vijana wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B kwa jinsi walivyojitoa katika kuhakikisha harusi inapendeza. Akiongea kwa furaha alisema, ilifika kipindi watu waliohudhuriia hariusi hiyo wakawa wanajiuliza "Imekuwaje mbona harusi imefana?".

Pia anamshukuru sana Mungu kwani mke wake amekubalika kwa asilimia zote katika kanisa lake la EFATHA Temeke kutokana na wema wake na kile alichokipanda katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Joseph alimpongeza Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa malezi bora na alimtabiria kuwa "Kila kuitwapo leo watu watao na kuolewa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwasababu Bishop anajua kulea watotoo wake kimwili na Kiroho."

Aliwashauri vijana wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuacha kuwa na macho ya "Chips" bali wanapotaka kuoa au kuolewa watazame roho zao zinasemaje na kumshirikisha Mungu, na wasikurupuke kuoa/kuolewa kwa kuangalia walivyopendeza au kuangalia vitu wanavyomiliki. 

Maria naye alimshukuru sana Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kumlea katika misingi bora. Alimshukuru Mungu kwa mkono wake uliokuwa juu yake akiwa katika kanisa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Alisema hakika amepata mume aliyekuwa akimuomba Mungu, na aliwashukuru wazee wa kanisa, vijana na kuwaombea Mungu awakumbuke katika mahitaji yao.

Hivi ndivyo wanandoa hawa walivyomshukuru Mungu. Yawezekana umehangaika sana kutafuta mume wa kufunga naye ndoa, kila ukijiangalia unaona umri unakwenda, umebaki ukilia na kukosa amani katika moyo wako. Ninakusihi, wewe muangalie huyu Mungu na usikose kushiriki ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili uweze kupata mafundisho ya Mungu na ahadi za Mungu kupiti watumishi wake. Jitahidi kupiga magoti na kuomba kutoka ndani ya moyo wako.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Kanisa limeandaa usafiri wa bure kutoka kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. baada ya ibada utarudishwa kituoni.















Comments