RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA WALIVYOMTUKUZA MUNGU KWA NYIMBO KATIKA IBADA YA KUSHIKWA MKONO NA MUNGU

Katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaya ya Joybringers na Happy kwaya za kanisani hapo zilifanyika baraka sana kwa nyimbo zao zenye kufundisha, kuadibisha na kuelimisha. Hakika tuliona uwepo wa Mungu kupitia waimbaji hawa kwa nyimbo zao na jinsi wanavyojituma katika kucheza kwa utukufu wa Mungu.

Waimbaji hawa ambao wamejitoa kwa kazi ya Mungu mara nyingi wamefanyika baraka kwa kanisa na kwa watu wanaofika katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa nyimbo zao zilizobeba ujumbe wenye kuleta uwepo wa Mungu  na nguvu za MUngu unapousikiliza. Baadhi ya watu wamekuwa wakipona na kufunguliwa kupitia waimbaji hao, wamekuwa wakifarjiwa na kutiwa moyo, imani zao zimekuwa zikijengeka kupitia waimbaji hawa. Hakika tunaona upendo wa Mungu kupitia wanakwaya hawa, Mungu anawatumia kwa njia ya aina yake kuhakikisha watu wake tunapona Kiroho na kubarikiwa kimwili.

Pengine ungetamani kuchota baraka zako kutoka kwa Mungu kupitia waimbaji hawa, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Na siku za katikati ya wiki ibada zinaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.  Mungu anakuita sasa ili abadilishe maisha yako, umeteseka vya kutosha na mambo ya kidunia.

Siku ya Jumapili kanisa limeandaa usafi wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.
Joybringers Kwaya






Happy Kwaya







Comments