RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.11.2017: WANANDOA WAMSHUKURU MUNFU KUFANIKISHA HARUSI YAO KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya KUVIKWA KIBALI iliyofanyika siku ya Jumapili 19.11.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", wanandoa wanaonekana kwene picha hapo chini walimshukuru Mungu kwa kuwapigania kuanzia kipindi chao cha maandalizi ya harusi mpaka walivyofanikiwa kufunga ndoa yao. Walishukuru Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatatare wa kuwalea kiroho na pia walimshukuru Mch. Noah Lukumay kwa mafundisho ya ndoa na bila kulisahau kanisa zima kwa ushirikiano wao.

Yawezekana umelia sana ukihitaji kuoa au kuolewa, tunakukaribisha katika ibada zetu hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi, ili tumlilie huyu Mungu na kumuomba kwaajili yako wewe unahitaji kuoa au kuolewa. Mungu wa kanisa hili ni mwaminifu na husikia maombi ya watu na kujibu. Mungu akutie nguvu ili Jumapili hii tukutanie katika nyumba ya BWANA









Comments