RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.11.2017: MAMA APATA MTOTO KIMUIJIZA WAKATI AKIWA NA MAUMIVU YA UGONJWA



Pamoja na changamoto za mke wake kusumbuliwa na ugonjwa lakini Mungu alimuwezesha mke wake kubeba mimba na leo anamshukuru Mungu kumpata mtoto. Mume wake akiongea katika ibada ya maombi ya KUVIKWA KIBALI iliyofanyika siku ya Jumapili 19.11.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alisema, kutokana na agano aliloweka na Mungu la kupata mtoto kipindi hana mtoto, hakushangazwa kuona mke wake amepata ujauzito wakati bado anasumbuliwa na ugonjwa wake. Yeye alibaki kumshukuru Mungu kwa kumpa mke wake ujauzito. Alisema haya yote yanatokana na maombi aliyoyaomba kipindi cha SHILO.

Yawezekana na wewe unahitaji mtoto na umehangaika bila majibu. Ninakuomba kipindi hiki cha kongamano la Shilo Tanzania 2017 la Mungu Kujifunua katika maisha yetu, usipange kukosa. Hii ni kongamano ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka na hukusanya maelfu ya watu kutoka kila kona ya dunia. Hudhuri kongamano hili ukiwa na IMANI ya kupokea jhaja ya moyo wako na ikiwezekana weka agano na Mungu wako. Kongamano hili litaanza Jumapili 3 hadi 10 Desemba 2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" saa 3 asubuhi kwa siku za Jumapili na katikati ya wiki ni saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.









Comments