RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: MUUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AMKUMBUKA MUNGU KWA KUMTOLEA MALIMBUKO

"Zaburi 117-Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele"

Muumini huyu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 17.09.2017 katika ibada ya KUKOMESHA UTASA aliweza kutoa MALIMBUKO ya mazao yake kwa Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili yaombewe.

Tunavyobarikiwa na Mungu, tukumbuke kumshukuru Mungu wetu na kumtolewa MALIMBUKO ya mavuno yetu.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada iliyojaa upako wa KIMUNGU itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Walete wenye shida mbalimbali, Mungu atawasaidia.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Baada ya ibada utarudishwa kutuoni.





Comments