RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: MAMIA WAOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

"ZABURI 22:1- Heri KUCHAGUA jina jema kuliko MALI nyingi; Neema kuliko fedha na dhahabu." Katika ibada MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya  Jumapili 17.09.2017, Mh. Bishop Dr. Grertrude Rwakatare aliwapongeza waongofu wapya walioamua KUCHAGUA JINA JEMA la Yesu Kristo kwa kuokoka na kuongozwa sala ya toba na baadae kubatizwa kwa maji mengi. Watu hawa wameona ni heri kuja kwa Yesu kuliko kuhangaikia UTAJIRI wa duniani na mwisho wa siku wakaikosa mbingu. Uamuzi wao ni uamuzi wa busara na wen ye kumpendeza Mungu na wadamu. 

Biblia inasema katika ZABURI 22:3- "Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha, bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Thawabu wa unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima." Watu hawa wameona mabaya yao na ndio maana wakaona ni vyema kujificha kwa Mungu ili wawe kwenye mikono salama na waondokane na kuitwa wajinga ambao husababisha wakaumizwa. Baada ya kuokoka na kubatizwa watu hawa wataheshimiwa na Mungu na watapata uzima udumuo kama Biblia inayosema, kwasababu wamekubali kwa nafsi zao kuokoka na kuacha mabaya.  Maumivu yanatokea pale tu shetani anapokuwa amewatawala na kuwaongoza jinsi atakavyo lakini mtu anapookoka hawezi kuogozwa na nguvu za giza bali anakuwa katika mikono salama ya Mungu na kulindwa na nguvu za Mungu.

Pengine wewe hujaokoka na unatamani kuokoka sasa, nafasi bado unayo, fika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Utaongozwa sala ya toa, utaombewa, utabatizwa na siku ya Jumatatu na Jumanne utaanza masomo yako ya kukulia wokovu ambayo huanza saa 9 alasiri.

Kama ni mara yako ya kwanza kufika, kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa. Ukifika hapo utasikia watu wakisema kanisani kwa Mama Rwakatare. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Mlete na mwingine. Ubarikiwe na BWANA
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare




















































 Mch. Asenga



Comments