RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: BAADA YA MIMBA KUPOROMOKA KWA MUDA MREFU, HIVI SASA AJIFUNGUA MTOTO KIMUUJIZA

MITHALI 16:5-7: "Kila mwenye MOYO wa KIBURI ni chukizo kwa BWANA, hakika hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za BWANA zikimpendeza BWANA, hata adui zake huwapatanisha naye.

Mama huyu kwa kipindi kirefu amekuwa akipata mimba lakini hazikai (zinaporomoka) lakini alipokanyaga katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kukutana na mtumishi wa Mungu Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mungu aliweza kumfuta machozi ya kuwapoteza watoto wake kutokana na mimba kuporomoka. Mungu alimuwezesha kushika mimba na mpaka akajifungua salama.

Yawezekana maadui zake walikuwa walimnenea maneno machafu ili azizae lakini BWANA alichukizwa mioyo ya maadui zake na akaweza kuwadhihirishia kuwa yeye ni Mungu wa mwenye haki. Unapomucha BWANA uovu hujisafisha na kuwa mbali na wewe, milango ya mafanikio inafunguka. Huyu dada baada ya kuamini kuwa Mungu anaweza na kumcha Mungu kwa roho ya kweli, aliweza kujipatia yule mtoto aliyekuwa akimtaka kwa muda mrefu. Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ni Mungu wa majibu chanya. Unatakiwa kuwa mvumilivu, mtu wa imani, mtu wa maombi, mtu mwenye upendo, kushika na kuzifanyia kazi amri kumi za Mungu, kutenda yaliyo mema, uwe mtu wa toba, soma Neno la Mungu likupe maarifa ya kujua siri za Mungu na mengine kama hayo.

Akiongea kwa furaha siku ya Jumapili 17.09.2017 alimshukuru sana Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, wachungaji, wainjilisti na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa maombi yao ambayo yamesababisha leo kupata mtoto na mimba haikuweza kuporomoka kama siku za nyuma kabla hajaanza kuabudu katika kanisa hili.

Pengine na wewe unapitia changamoto kama hizo, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana ukutane na nguvu za Mungu.























Comments