RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

10.09.2017: MATUKIO KATIKA PICHA YA UZINDUZI WA KONGAMANO LA WANAWAKE LITAKALOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya KUKOMESHA UTASA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 10.09.2017 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Wanawake au Wamama wa kanisa hili waliweza kuzindua rasmi KONGAMANO LA WANAWAKE KITAIFA / WOMAN OF CHRIST (WOC) amba litaanza tarehe 24.09.2017 hadi 01.10.2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri hadi uskiy

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. aliwashukuru wamama na kusema wanawake ni tunu na ndio maana utaona kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walio wengi ni wananwake. Alisema wamama ni watu muhimu sana katika familia na taifa kwa ujumla, wana mchango mkubwa katika maendeleo ya wababa na maendeleo ya taifa, wamama ni wachapakazi, watu wenye moyo wa huruma na upendo.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kutoa dondoo za vitu vitakavyofanyika katika Konagamano hili la Wanawake, ambazo ni:-

1. Kukomesha umaskini kwa mwanamke na kumuinua Kiuchumi. kupata mitaji
Kukopeshana, kuhakaikisha mwanamke anakuwa tegemezi katika familia, kum-empower na kumuweka strong mwanamke "financially"

2. Kutakuwa na maombi ya kina ya uzao wa tumbo la mwanamke. Wale wenye shida ya kupata watoto na ambao mimba zao hazikae wataombewa na kufunguliwa

3. Kukomesha kilio katika ndoa za watu. Wale waliokosa amani katika ndoa zao kutokana na ukorofi wa mwanaume au mwanamke mwenyewe kuwa mkorofi kwa mume wake. Ukorofi wa ndugu wanaotamani kuharibu ndoa za watu, ukorofi wa marafiki wenye nia ya kuharibu ndoa za watu. Kukomesha kilio cha mwananmke ambaye anaishi na mume wake ambaye hajaokoka

4. Kuombea huduma za wamama. Wapo wengine wamepewa huduma kwaajili ya kazi ya Mungu lakini hawazitumii.

5. Kukomesha kilio cha magonjwa kwa wanawake kama vile UKIMWI, kansa, pressure, TB, vidonda sugu, kupooza, kutokwa na damu, magonjwa ya moyo, BP n.k

KWAHIYO USIKOSE KONGAMANO HILI KWA FAIDA YAKO NA FAMILIA YAKO NA TAIFA KWA UJUMLA











































































Comments