RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

03.09.2019: MATUKIO KATIKA PICHA YA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KATIKA IBADA YA KUPOKEA HABARI NJEMA

Ilikuwa ni siku ya Jumapili 03.09.2017 katika kanisa linalopendwa na wengi la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuhubiri juu ya kupokea Habari Njema kutoka Kwa Mungu mwenyewe. Watu wengi sana wamekuwa wakipokea habari mbaya kama vile habari za magonjwa, ajali, kuachika, kutozaa, kutooa au kuolewa, kulonwa, kutupia majini na mapepo, kufukuzwa kazi, kutothaminiwa nyumbani au kanzini na zingine kama hizo.

Kupitia ibada ya KUPOKEA HABARI NJEMA watu wengi walifunguliwa katika ulimwengu wa kupokea Habari Mbaya. Bishop Dr. Gertrude Rwaklatare aliwaombea na kuwatamkia yakuwa ndani ya miezi mitatu iliyobaki watu watakuja na shuhuda zao mbalimbali walizotendewa kabla ya mwaka 2017 kumalizika.

Watu wengi wamkuwa wakifunguliwa kutoka kwenye nguvu za giza zilizoharibua kazi zao, biashara zao, nyumba zao, ndoa zako mahusiano yao na mengine kama hayo.

Katika kitabu Warumi 8:8-9, Mungu anasema, " Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, nanyi hamfuati mwili; bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake..."Kwahiyo Roho wa Mungu ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, na Roho wa Mungu hukaa ndani ya mtu aliye safi kiroho. Dhambi na matendo mabaya yanweza kusababisha ndani ya mwili wako mkawa mchafu na kutokana na uchafu ukasababisha hata Roho wa Mungu kutokuwa ndani yako.

Roho wa Mungu hutuongoza kwa kila jambo tunalolifanya, au tunalotaka kulifanya. Unapoanza kufanya jambo baya, Roho wa Mungu hutukumbusha kuwa hilo jambo sio zuri kulifanya kwahiyo nafsi yako inaweza kuamua kulifanya au kutolifanya. 

Kwahiyo kama watu tuliokoka na tunampenda Mungu hatupaswi kuyafuata sana ya mwili, kwani tunayozidi kuyafuata ya mwilini na kusahahu ya rohoni, hatumpendezi Mungu wetu aliyetuumba na kutupa uhai huu tulionao. na kama tunataka kuwa wana wa Mungu tunatakiwa kuwa na Roho wa Kristo.

Endelea kufuatilia Post zeu. Tunaandaa somo la Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare la Jumapili 

Tunakukaribisa katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni i"B". Ibada itanza 3 asubuhi

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare














































































































Comments