RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: RAIS MAGUFULI AMTUMBUA HADHARANI HAKIMU HANDENI -TANGA

TANGA: Rais Magufuli ameagiza Hakimu wa Mahakama ya Mazingara wilayani Handeni mkoani Tanga aliyetajwa kwa jina moja la Laizer ahamishwe mara moja kwa kushindwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Hayo ameyaagiza leo wakati akizungumza na wananchi wa Manga wilayani Handeni alipokuwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani humo.

Wakitoa malalamiko yao,wakulima wa eneo hilo walimueleza Rais kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na wafugaji kwa kulishiwa mazao yao na wakipeleka malalamiko ya mahakamani hawapati haki zao..

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe alikiri kuwa, ni kweli hakimu huyo amekuwa hatendi haki, anapendelea upande mmoja wa wafugaji. hivyo kuwa kikwazo kikubwa kwa maendelo ya wakulima kwa kushindwa kutatua migogoro hiyo.

MSIKIE RAIS AKIMTUMBUA HAKIMU

Comments