RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHRISTOPHER MUHANGILA AKONGA MIOYO YA WATU KWA WIMBO WAKE MPYA SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Christopher Muhangila alifanyika baraka katika ibada ya KUKATA RUFAA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 06.08.2017. Katika ibada hii tuliona Mungu akishughulika na maisha ya watu klupitia huduma ya mtumishi huyu, nyimbo yake ilileta uwepo wa Mungu kabla ya mtumishi wa Mungu Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuanza kuhubiri. Hakika mtumishi huyu BWANA anamtumia kwa viwango vya tofauti sana. Mungunazidi kulinda karama yake na huduma yake aliyonayo ili watu wengi wapate kumjua huyu BWANA wetu Yesu Kristo. Nasi tunamuombea maisha marefu na kanisa linampenda kwa kazi nzuri anayofanya kwaajili ya kuokoa roho za watu kupitia uimbaji wake.
06.08.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": CHRISTOPHER MUHANGILA
Mungu afungue milango ya mafanikio na baraka tele katika familia yake, huduma yake ikafanyike ibada kwa kila mtu atakayesikia nyimbo zake. Hatuna la kusema juu ya mtumishi huyu ila tunamuombea sana ili kazi ya BWANA isonge mbele kupitia uimbaji wake.

Nikukaribishe Jumapili hii kwako wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada ya Jumapili hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada hii itabadilisha historia ya maisha yako. Fika hapa kanisani ukiwa na IMANI ya kupokea majibu kutoka kwa Mungu mwenyewe kupitia watumishi wake. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na jopo la wachungaji wamejiandaa kwaajili ya kushughulika na maisha yako. kwahiyo usipange kukosa kabisa. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri ni bure kuuanzia kituo cha Mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni.










Comments