RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

30.07.2017: WAUMINI WAKIPITISHA VIFAA VYA KUPIGIA MAGOTI WAKATI WAKUOMBA KWA MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ILI VIOMBEWE

Katika ibada ya KUUNGANISHA NYUMBA ZETU NA MADHABAHU YA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 30.07.2017 waumini na wageni waliofika kuabudu mahali pale walileta vifaa maalum kwaajili ya kupigia magoti wakati wa maombi majumbani mwao ili viweze kuombewa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Baada ya kuombewa waumini na wageni waliweza kupita madhabahuni kujiunganisha na madhabahu ya Mungu na madhabahu ya majumbani huku wakisalimiana na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kuwatamkia baraka.

Mh. Bishop Dr. Gertrude aliwaomba watu kuwa na vyumba maalum majumbani mwao kwaajili ya kufanyia maombi. Aliwaomba sana watu kuwa na ibada za majumbani, aliwaagiza kila mtu aje na kifaa cha kupigia magoti wakati wa maombi ili kiombewe na na kujiunganisha na madhabahu ya Mungu iliyopo kanisani. Watu walikuja na vitenge, vilago, mashuka, vitambaa, vibao n.k. kila mtu alileta kile anachoona kwake kinaweza kumsaidia kupigia magoti wakati  akifanya maombi na Mungu katika vyumba vyao. Bishop aliwaomba watu wanaoishi nyumba za kupanga wakati  wa maombi wajaribu kuwahi mapema kabla ya watu hawajalala ili kuepusha usumbufu kwa watu wenye imani tofauti, kwani kuna watu wengine wanavyoomba wanatoa sauti kubwa.

Pengine ulikosa ibada ya Jumapili, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.





































































Comments