RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

20.08.2017: MAOMBI YA KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA WABAYA WETU YALIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI


Mungu anazidi kuwashangaza watu wanaohudhuria ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku za Jumapili na katikati ya wiki. Tumekuwa tukishuhudia watu wakitoa shuhuda zao jinsi Mungu alivyowatendea katika maisha yao. Inafika kipindi mtu haamini yale anayotendewa katika maisha yake. Mungu wetu wa mbinguni ni Mungu wa kushangaza watu wake. Amekuwa mwaminifu, mwenye upendo, mwenye huruma, msikifu, anatenda kwa wakati, anasikia maombi ya watu na kuyatimiza kwa wakati apendao Yeye.

Mungu huyu anaweza kutenda hata kwako kama utamkubali na kuishi kama Yeye apendavyo kwa kusoma Neno lake, kuyafanyia kazi unayosoma, na kuishi maisha mema, kuvumilia na kupambana kiroho changamoto zinapokujia, kutokata tamaa, kushiriki ibada, kuwa mtoaji kanisani, kuwapenda watu wote, kusaidia wenye uhitaji, kushika amri za Mungu na kuzifanyia kazi na kutnf=da yale yote mema kwa kila mtu.

Siku ya Jumapili 20.08.2017 katika ibada ya KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU WASIOPENDA MAENDELEO YETU, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay na jopo la wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kufanya maombi maalum ili Mungu aweze kutgua mitego ilitegwa na wabaya wetu ili tusifanikiwe kiuchumi. Maadui zetu wametunenea maneno mabaya katika vyanzo vya mapato yetu, wameenda kwa waganga na kutuloga ili milango ya fedha ifungwe na tunbaki kuwa maskini, wamepaka matope nyota zetu za mafanikio, vibali vyetu, kazi zetu, wateja wetu n.k. Tumebaki watu wa kuhangaika na inafika kipindi tunakata tamaa kama wanadamu kutokana na umaskini unaotunyemelea katika maisha yetu pamoja na familia zetu.

Tunamshukuru sana Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kupata maono ya kufungua milango yetu ya mafanikio ambapo aliwaomba watu washike pochi zao, mikoba yao, wailet zao, funguo zao na akafanya maaombi maalum ya kumuomba mwenyezi Mungu afungue milango wa pesa kwa waumini hawa.

Watu walijiachia kwa Yesu Kristo kwasababu yeye ndiye kimbilio la wengi. Ibada hii iligusa hisia za watu wengi sana kutokana na uwepo wa Mungu uliotanda kanisa zima. watu waliguswa na nguvu za Mungu na wengi kuanza kupiga kelele, kutoa machozi ya furaha.

Katika kanisa hili tumeshuhudia watu wengi wakija hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa hawana magari, nyumba, viwanja, wachumba wa kuwaoa, kazi, kibali, promosheni kwao ni shida, afya zao migogoro, hawapati tenda, pesa wanapata za kula tu, ndoa zao ni shida, wanateswa na nguvu za giza, wachawi wanawachanja chale usiku, hawana mafanikio, ndoto chafu zinawasumbua, kule kuhushimiwa kwa mara ya kwaza hakupo tena, lakini wanapofika katika nyumba ya BWANA na kufundishwa Neno la Mungu ili waweze kujisimamia kupambana na changamoto, wengi wao wamefanikiwa na wanamshukuru Mungu kwa wema mkuu.

Pengine na wewe unatamani kupata "Breakthrough" katika jambo unalopitia, tunakukaribisha katika ibada ya Jumatano saa 9 alasiri, Ijumaa saa 9 alasiri na Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako.

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


Mch. Noah Lukumay





























Mch. Stanley Nnko

Janeth Urasa

Mzee wa kanisa Mulele

Mchungaji kutoka Congo

Mch. Elizabeth Lucas





Furaha Isaya



























Comments