RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

20.08.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA IBADA YA KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU KATIKA MAISHA YETU ILIYOFANYWA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mlima wa Moto, Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Mountain of Fire, Mountain of Fire Tanzania, Mama Gertrude Rwakatare, Mch. Gertrude Rwakatare, Askofu Gertrude Rwakatare, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mlima wa Moto Tv, Rumafrica,Rumafrica online Tv, Rulea Sanga, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Getrude Lwakatare, Gertrude Lwakatale, Lwakatare, Mch. Getrude Lwakatare

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku ya Jumapili 20.08.2017 katika ibada ya "KUFUNGUA MILANGO AMBAYO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU KATIKA MAISHA YETU ILI TUSIFANIKIWE" watu wengi sana walijitokeza madhabahuni kwaajili ya KUOKOKA. Mch. Noah Lukumay na Mch. Francis Machichi waliwaoongoza sala ya toba, waliwaombea na baada ya ibada kumalizika wainjilisti na wachungaji mbalimbali waliwabatiza kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku yao ya kujifunza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri. 

Ndugu yangu wewe ambaye hujabatizwa na kuongozwa sala ya toba, Mungu anakuhitaji, anatamani kukuona unaishi maisha matakatifu ili siku ya mwisho ya kuishi hapa duniani ukaonane naye huko mbinguni. Unatakiwa kutambua kuwa hujui kesho yako, anayejua ni Mungu wako, hujui baya gani litakukumba baada ya kuondoka hapo ulipo, unatakiwa kujiuliza kuwa baada ya maisha ya hapa duniani nini kitafuata? Sauti ya Mungu inakuita sasa...OKOKA na umtumikie Mungu.

Pengine unatamani kuokoka, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Watumishi wa Mungu wakiongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wanatakuombea na kukuongoza sala ya toba na utabatizwa kwa maji mengi siku hiyo hiyo. Mungu akubariki sana..

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumatano saa 9 alasiri, Ijumaa saa 9 alasiri na Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako.


Mch. Noah Lukumay akiwaongoza sala ya toba na kuwaombea waongofu wapya.






















Comments