RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

20.08.2017: MAOMBEZI YA KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU YALIVYOAFANYIKA MLIMA WA MOTO SIKU YA JUMAPILI

Hakika Mungu ni Mungu wa milele. Tunahitaji kujipendekeza kwake ili tupate usalama wa Roho zetu. Huyu Mungu atabaki kuwa Mungu kwani anayofanya katika maisha ya wanadamu ni makubwa sana. Anawapenda wanaomsaliti, anawapenda wanamtii na kumfuata. Mungu wetu hana upendeleo kabisa, ni Mungu wa huruma na upendo. Tumfaute Mungu wetu daima ili tupate kujua jinsi alivyo, tutembee naye na kumuishia milele kwani yeye ni Mungu mtakatifu, na ni Mungu wa kusifiwa. Tunatakiwa kujiuliza baada ya maisha ya hapa duniani, tunauhakika wa kuonana naye huko mbingnuni? Kama unaona huna uhakika wa maisha ya baadae, basi anaza kuyaandaa sasa ili usiingie motoni siku ya mwisho. Jitahidi sana kufanya maombi na kutenda yaliyomema tu.

Katika safari ya maisha yetu bila ya Mungu hatutaweza, kwani maisha yetu ni kama mvuke na yananyauka kama maua. Mungu anajua maisha ya wanadamu kwani ametutoa mbali, ametuvusha katika mabonde na milima, anaiishi na watu wa kila namna. hakika Mungu pekee ndiye mtakatifu.

Wanadamu wakijingamba na kujivuna hawajui kuwa Mungu ni Mungu wa milele, na ndiye aliyewaumba na kuwaleta hapa duniani, hawajui kuwa Mungu ana uzoefu wa kutosha, anaweza kukunyima hiyo pumzi au kukuachia hiyo pumzi, kwahiyo tunatakiwa kuwa wanyenyekevu mbele zake.

Tunamshukuru Mungu kwa siku ya Jumapili tumemuona Mungu akishughulika nasi katika ibada ya KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA NA MAADUI ZETU ILI TUSIFANIKIWE. Katika ibada hii Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la Wachungaji waliongoza kipindi cha maombezi. Kila aliyefika katika ibada hii aliweza kuwakilisha shida zake kwa Mungu aliye juu.

Tunajivunia kuwa na huyu Mungu kwani tumeona akijibu maombi ya watu. Kila tuombalo Mungu amekuwa mwepesi kutupatia. Kuna watu walikuja Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa hawana pesa, hawana nyumba, hawana viwanja, hawajaoa/kuolewa, wanadaiwa, hakuna amani katika ndoa, wanateseka na wachawi, roho chafu zimewaandama, mapepo yameweka makazi katika miili yao na shida mbalimbali kama hizo, lakini walipokutana na mkono wa Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" shida zao zikaanza kuondoka na sasa wanafurahia wema wa Mungu.

Yawezekana na wewe ulitamani kushiriki maombi haya lakini kutokana na sababu zisizozuilika hukuweza kufika kanisani, nataka nikwambia nafasi bado ipo, jitahidi kufika mapema Jumapili hii saa 3 asubuhi ili ukutana na wema na huruma za Mungu katika maisha yako.

Unatakiwa kuwa na IMANI (FAITH), ujitakase kwa kutubu dhambi zako, uyatende matendo mema ya Mungu, ushiriki ibada za Mungu, ujifunze Neno la Mungu na kuyaishi yale unayojifunza, kusoma Biblia na kuishi kama unavyoaagizwa kwenye Biblia, uwe na upendo, uachane na maovu na uishi maisha mema, uwe mtoaji kanisani, uyatii maagizo ya watumishi wa Mungu, uwe muombaji sana n.k.. Ukiyafanya hayo yote na mengine ambayao sijayasema, utaona mkono wa Mungu katika maisha yako na utakuwa na uhakika wa kuingia mbinguni. Usikubali kudanganywa na Roho chafu sinazokuambia usitende mema. Mungu akubariki sana.

Sasa, pengine na wewe unatamani kupata "Breakthrough" katika jambo unalopitia, tunakukaribisha katika ibada ya Jumatano saa 9 alasiri, Ijumaa saa 9 alasiri na Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Njoo na rafiki yako.


Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare
















































Mch. Stanley Nnko




Mch. Alex














Comments