RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.08.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Eee Mungu ni mwema sana katika maisha yetu, tunaona mkono wako katika mihangaiko yetu, unatubariki na kutulinda. Wewe ni wa kuabudiwa na kutukuzwa kwasababu unastahili katika maisha yetu. Umetubariki na hakuna aliyeweza kutuzuia. Ulisema tukiweka tumaini letu utabadili historia yetu, nasi leo tumeona ukibadilisha maisha yetu kutoka katika umaskini wa kimwili na kiroho na kuwa matajiri wa kimwili na kiroho. Tunakuabudu wewe Mungu kwasababu ya upendo wako na upole wako, wewe Mungu ni mtakatifu, mnyenyekevu kwetu. Umebadilisha maisha ya walio wengi na sasa wanafurahia ukuu wako. Baba tunakuabudu na kukutukuza kwasababu unastahili Baba yetu wa mbinguni. Tumekuona Ee Mungu siku ya Jumapili 06.08.2017 katika ibada ya KUKATA RUFAA iliyofanyika katika hekalu lako la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Umemtumia mtumishi wako Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kama chombo cha kupitisha ujumbe wako wenye faraja kwetu. Hakika Mungu unastahili kusifiwa na kuinuliwa kwa yale unayofanya katika kanisa lako la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Umewafunguwa waliofungwa katika ndoa zao, familia zao, kazi zao, majumbani mwao, mashambani mwao, afya zao, safari zao, masomo yao, mahusiano yao, uchumba wao na kila eneo Mungu tumeona mkono wako wenye upanga wa moto ukikata minyoyoro ya adui shetani. Mungu tunakupenda sana kwa kutupa watumishi wako wenye kulitii andiko lako na ktuongoza katika nia sahihi ya kuufikia ufalme wako. Mungu tunayofuraha, tumaini, amani tunapokuwa na wewe kwasababu wewe ni mtetezi wetu na uko hai unaishi milele. Tunajivunia kuwa na wewe MUNGU wetu. Baba tusamehe pale tunapokukosea, tufutilie mbali na yale maovu tuliyokukosea kwa kujua au kutokujua. Ee Mungu wewe ni Mungu wa kusamehe, tunaamini na siku ya leo unakwenda kutusamehe BABA. Angalia walio katika changamoto mbalimbali, tunaomba BABA uwaguse na kuwasaidia kufanikisha kwa kile wanachokitafuta. Mungu wewe ni mwaminifu, na hujawahi kusema uongo katika maisha yetu. Tunakutukuza ee Mungu kwa ukarimu wako na hekima zako. Sasa niongee na wewe ambaye unatamani kufika katika ibada zetu za Jumapili za Mlima wa Moto Mikocheni "B", ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni. Usikose ibada hii itakayokuondoa hapo ulipoa na kukupeleka mahali ambapo utasema "Hakika Mungu ni Mwema." Ni siku ambayo mateso yako yatakwenda kuondolewa kwa damu ya Yesu Kristo. NB: Tunaomba uendelee kufuatilia post zetu. Tunakuandalia somo la Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alilojubiri siku ya Jumapili 06.08.2017. Mungu ana akubariki sana.

 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare






























Comments