RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TANZIA: JAJI UPENDO MSUYA AFARIKI DUNIA

Upendo Msuya enzi za uhai wake.

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye alijiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akithibitisha kifo hicho, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwaHospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga



Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

Comments