RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EFATHA MINISTRY: ZIARA YA KITUME NA KINABII EFATHA MINISTRY - MKOA WA MARA SOMO: UBABA

Nabii na Mtume Josephate Mwingira

Mathayo 11: 25, "Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia".

UBABA ni tofauti na kuwa mzazi, UBABA ni ROHO au TABIA; Bwana Yesu akasema nakushukuru Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili ukawafunulia watoto wachanga.

UBABA ndio wenye kufunua SIRI; Unatangaza UBADAE wa Mtu na UNAFUNUA mambo yaliyofichika. Mfano kabla mtu hajafa ubaba unafunua siri ndio maana mtu anasema shamba hili ni la mtu fulani, nyumba hii niya fulani, wewe ulijua ni yakwako kumbe ana siri moyoni mwake.

Huyu Baba ambaye nataka ujue habari zake ni Bwana wa Mbingu na nchi. Kuna watu wana akili na hekima na ni Mungu mwenyewe amewapa ila kuna mambo amewaficha na amewafunulia watoto wachanga. Anaposema watoto wachanga anamaanisha watu ambao ni wanyonge, wasio na majina, wasio tambulika na wasio pewa heshima, hao ndio anao wafunulia.

"Kumfahamu Mungu inatokana na mapenzi yake maana yeye ndiye anaye kufunulia".

Unaweza kutembea hapa duniani mpaka ukafa pasipo kumjua Mungu, unaweza kwenda kanisani miaka mingi na ukawa humjui Mungu. Kuna watu wanafundisha kwenye masinagogi lakini hawamjui Mungu, ndio maana hawakuweza kukusaidia mpaka ulipokuja kwa wanaomjua Mungu wakakusaidia ukafunguliwa.

Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - Efatha Ministry.

Comments