RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

16.07.2017: WALIKOKA KATIKA IBADA YA KUPELEKA MASHTAKA KWA MUNGU ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 16.07.2017 katika ibada ya KUEPELEKA MASHITAKA YETU KWA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ikiongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, watu wengi walijitokeza kuokoka. Wachungaji waliweza kuwaombea, kuwaongoza sala ya toba na baadae kubatizwa kwa maji mengi. Wakati wakiombewa wengi wao walitokwa na mapepo , majini na roho chafu zilizokuwa zikiwasumbua kwa kipindi kirefu sana. 

Siku ya Jumatatu na Jumanne waliendelea na masomo yao ya kukulia wokovu ambayo hutolewa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri. Katika darasa hili wanajifunza mambo mengi kuhusu Mungu, jinsi ya kutunza wokovu wako, mambo ya imani, kuwajua baadhi ya wachungaji na watumishi wa kanisa, tabia njema, masomo ya kujisimamia mwenyewe katika wokovu, kumjua Mungu, jinsi ya kusali na mambo mengi za ya Kimungu.

Katika kanisa hili kumekuwa na mwitikio mkubwa sana wa watu wanaokoka na kubatizwa, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwaokoa hawa watu. Pia tunawashukuru wachungaji, wainjilisti na wahudumu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kujituma kwao kwenda mitaani kulitangaza Neno la Mungu. Juhudi zao zimeleta matunda na ongezeko la watu wanaokoka. Pia hata wewe ulipo unaweza kuwa balozi wa Yesu kwa kulihubiri Neno la Mungu kwa majirani zako au familia yako, watangazie Injili nao wataguswa na nguvu za Mungu na baadae wataamua kuokoka. Kazi hii ya kuhubiri si kwa wachungaji bali ni kwa watu wote. Unachotakiwa ni wewe kulijua Neno la Mungu kiundani zaidi kwa kusoma Neno lake ili likuongoze katika huduma unayofanya ya kutangaza habari njema za Yesu Kristo. Mungu amekuumba ili ufanye kazi yake kwa moyo wako wote kupitia karama uliyonayo.

Sasa, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, ukifika hapo utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"








































Comments